Quantcast
Channel: TAMWA - TAMWA - PRESS RELEASE
Viewing all articles
Browse latest Browse all 40

TAMWA YAUNGANA NA WADAU KUADHIMISHA SIKU YA UKEKETAJI DUNIANI

$
0
0
Chama cha Wanahabari Wanawake nchini – TAMWA kinaungana na mashirika mengine yanayopinga vitendo vya ukatili wa kijinsia na kutetea haki za binadamu leo tarehe 6 Februari, 2017, kuadhimisha siku ya Kimataifa ya kupinga ukeketaji duniani.   Kauli mbiu mwaka huu ni “Ujenzi wa daraja shirikishi na imara kati ya Afrika na Dunia kuondoa ukeketaji ifikapo mwaka 2030” (“Building a solid and iteractive bridge between Africa and world to accelerate ending FGM by 2030) ambapo kwa mujibu wa utafiti wa Kiafya wa demografia wa (TDHS-MIS) mwaka 2015-16, umeeleza kuwa mwanamke mmoja kati ya kumi amekeketwa licha ya elimu ya kuhusu madhara ya ukeketaji kuendelea kutolewa kwa jamii kila mara   Utafiti huo umebaini kuwa, uelewe kuhusiana na ukeketaji unaongezeka kadri kiwango cha elimu kinavyoongezeka kutoka asilimia 71 ya wanawake hadi kufikia asilimia 97. Aidha, utafiti huo umebaini kuwa kiwango cha wanawake wenye umri kati ya miaka 15-29 waliokeketwa kimepungua kutoka asilimia 18 mwaka 1996 hadi asilimia 10 kwaka 2015.   TAMWA inaamini kuwa ukeketaji unaweza kuisha endapo jamii itapata elimu endelevu ya kuondokana na mila kandamizi kwani zinakiuka haki za binadamu na kudhoofisha afya za wasichana na wanawake kwa kutokwa damu nyingi kwa wanaokeketwa na hadi kusababisha kifo, madhara ambayo hurudisha nyuma juhudi za kimaendeleo ya familia na Taifa kwa ujumla.   Aidha TAMWA inaamini kuwa vyombo vya habari vina nguvu kubwa katika kuleta mabadiliko katika jamii ikiwemo vitendo vya ukeketaji na aina zote za ukatili wa kijinsia     Edda Sanga Mkurugenzi Mtendaji.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 40

Trending Articles