Chama cha Wanahabari Wanawake – TAMWA kwa kushirikiana na Ubalozi wa Canada hapa nchini, leo Ijumaa tarehe 29 Januari, 2016 saa 08:00 asubuhi kitafanya mkutano wa siku moja kujadili yaliyojiri katika kongamano la nchi za Africa lenye lengo la mpango mkakati uliojadiliwa kwa ajili ya kutokomeza mimba za utotoni lililofanyika hivi karibuni Desemba, 2015 Lusaka nchini Zambia.
Mkutano huo ambao utafanyika katika ofisi za TAMWA Sinza Mori, Dar es Salaam, utahusisha pia wadau mbalimbali wanaopigania haki za watoto, kujadili ufanisi na utekelezaji wa sheria zilizopo ili kuweka mpango mkakati wa kulaani ndoa za umri mdogo hapa Tanzania na jinsi ya kusonga mbele.
Mkutano huo utajenga imani ya pamoja kutokana na maazimio ya kongamano la Umoja wa nchi za Afrika kwa kuwa Tanzania inatambua kuwa kutokomeza ndoa za utotoni kunahitaji dhamira ya kisiasa, yenye maono na uwezo wa kuongoza, ushiriki wa wadau mbalimbali, watoto, pamoja na uwezeshaji katika kupinga mila kandamizi kuanzia ngazi za chini ili kubadilisha taratibu ambazo husababisha kuongezeka kwa ndoa za umri mdogo.
Katika miaka ya nyuma na hivi karibuni kumekuwa na ongezeko la uhitaji mkubwa wa serikali na mashirika mbali mbali duniani kutaka kutatua tatizo la mimba za umri mdogo kama vile kutolewa kwa Mkataba wa Kutokomeza aina zote za Ukatili dhidi ya Wanawake (CEDAW) na Itifaki ya Maputo ambayo inakataza ndoa za utotoni. Hivyo ahadi, maazimio na mikataba hii inapaswa ifanyiwe kazi kwa vitendo ili kuleta mabadiliko ya kweli katika maisha ya
wasichana.
Edda Sanga
Mkurugenzi Mtendaji
PRESS RELEASE
TAMWA MEET WITH STAKEHOLDERS TO DISCUSS THE WAY FORWARD AFTER THE AFRICAN GIRLS SUMMIT ON ENDING CHILD MARRIAGE
The Tanzania Media Women’s Association-TAMWA in collaboration with the High Commission of Canada will today, Friday 29th January, 2016 from 08:00am conduct a one day meeting to carry forward lessons learned from the African Girls’ Summit on Ending Child Marriage held in Lusaka Zambia early December, 2015.
The meeting that will be held at the TAMWA Office, Sinza Mori, Dar es Salaam will involve other stakeholders campaigning for Children’s Rights to discuss more effective enforcement of existing laws that condemn child marriage in Tanzania and strategize the way forward.
The meeting will build on the spirit of African Union Summit where Tanzania recognizes that Ending Child Marriage requires political commitment, visionary and able leadership, and engagement of different stakeholders, children and support for grassroots advocacy to address many of the negative cultural practices and behaviours that place girls at increased risks of child marriage.
Child marriage is a human rights issue: a violation of human rights and a serious barrier to girls and women development. In Tanzania on average, two out of five girls get married before their 18th birthday, while in the African continent over 42% of girls are married before they reach 18 years, with millions of girls given away to marriage before they reach puberty. 31 out of 41 countries in the world, where prevalence rates of child marriage are more than 30%, are in Africa.
Edda Sanga
Executive Director