Quantcast
Channel: TAMWA - TAMWA - PRESS RELEASE
Viewing all articles
Browse latest Browse all 40

TAMWA: SHERIA YA USALAMA BARABARANI IFANYIWE MAREKEBISHO

$
0
0
Chama cha wanahabari wanawake tanzania -TAMWA kinaungana na watanzania katika maadhimisho ya nne ya umoja wa mataifa ya wiki ya usalama barabarani (UN Road Safety week) yatakayoadhimishwa kuanzia tarehe 08/05 na kufikia kilele tarehe 14/05. Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni “udhibiti wa mwendo kasi kwa vyombo vya vya usafiri”  TAMWA inawaasa wadau wa usalama barabarani wakiwemo Wabunge  kuadhimisha wiki hii kwa kupaza sauti na kutoa wito wa kufanyiwa marekebisho ya sheria na kanuni za usalama barabarani hasa sheria ya usalama barabarani ya mwaka 1973. Maeneo ambayo yanapaswa kuzingatiwa katika marekebisho ni mwendo kasi,  ulevi wakati wa uendeshaji, uvaaji kofia ngumu, kufunga mikanda na vizuizi kwa watoto.  Kutokana na idadi kubwa ya vifo na ajali  barabarani ambavyo hutokea kwa kiwango cha kutisha nchini.  TAMWA inaona kuna umuhimu wa kuchukulia jambo hili kama dharura kwa kuzifanyia marekebisho sheria na kanuni za usalama barabarni ili kuipa nguvu sheria hiyo kuwadhibiti wanaokiuka matumizi sahihi ya barabara.  Wakati tunadhimisha wiki ya umoja wa mataifa ya Usalama Barabarani, tumeshuhudia matukio mbalimbali ya ajali ambayo chanzo chake kikubwa ni makosa ya kibinadamu. Mfano wa tukio ni la tarehe 6 Mei, wiki iliyopita ambapo watanzania walipatwa na simanzi pale ambapo wanafunzi 32 na waalimu wao wawili pamoja dereva walivyopata ajali na kufariki papo kwa papo.  Madhara yatokanayo na ajali za barabarani yamemeendelea kuwa sababu namba tisa katika kusababisha vifo vya watu wengi zaidi duniani ambapo inakadiriwa zaidi ya watu milioni 1.25 hufa kila mwaka kutokana na ajali za barabarani.Wakati huo huo watu zaidi ya milioni 20 hadi 50 wamebaki na majeraha makubwa na aidha ulemavu wa kudumu kutokana na ajali hizi kwa mwaka. Kwa mujibu ya repoti ya haki za binadamu kwa mwaka 2016, ajali za barabarani zilipungua kwa nusu ya kwanza ya mwaka 2016, ikilinganishwa na kipindi kama hicho hicho kwa mwaka 2015 ambapo jumla ya ajali 5,152 ziliripotiwa kwenye Jeshi la Polisi kuanzia Januari hadi Juni 2016. Pia takwimu zinaonyesha kuwa kila mwaka watu 3,000 hupoteza maisha kutokana na ajali za barabarani Nchini. Edda sanga, Mkurugenzi mtendaji wa TAMWA anasema "Umoja wa mataifa na shirika la afya duniani wanakiri kwamba sheria  madhubuti zinahitajika katika kupunguza idadi ya watu wanaofariki katika barabara zetu. Tanzania lazima tuwe na sheria kali za usalama barabarani kukomesha hali hii . Lakini pia kwa mda wa miaka mitatu iliyopita Nchi karibia 17 zinazowakilisha wananchi milioni 409 zimetunga na kufanyia maboresho ya sheria angalau kwa kiashiria kimoja au zaidi ambavyo vimekuwa ndio vyanzo vikubwa vya ajali na Nchi hizo zimekuwa zikifanya vizuri katika kudhibiti ajali, ila Tanzania haipo miongoni mwa nchi hizo. Ni mda mwafaka sasa Tanzania kuchua hatua kwa matendo”. Edda Sanga Mkurugenzi Mtendaji

Viewing all articles
Browse latest Browse all 40

Trending Articles