Quantcast
Channel: TAMWA - TAMWA - PRESS RELEASE
Viewing all articles
Browse latest Browse all 40

TAMWA YAMLILIA DR. SUBILANGA KAGANDA

$
0
0
Chama cha Wanahabari Wanawake nchini (TAMWA) kimepokea kwa masikitiko kifo cha aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Wanawake Madaktari Tanzania (MEWATA) Dr. Subilanga Kaganda kilichotokea Jumatano tarehe 17/05/2017 huko APPOLLO nchini INDIA.  Kifo cha Dr. Kaganda kimeacha pengo kubwa ambalo halitasahaulika kamwe kwani alikuwa mtetezi mahiri, shujaa aliyefanya kazi kwa upendo, huruma na weledi usio kifani na alijipambanua kuwasaidia wanawake wa hali zote dhidi ya saratani ya mlango wa uzazi na matiti ambazo zimekuwa kero kwa wanawake wengi mijini na vijijini hapa nchini.  TAMWA inaungana na Watanzania wengine kutoa pole katika kipindi hiki kigumu kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki, madaktari na wanachama wote wa MEWATA.  Aidha wakati TAMWA tukiwasihi familia, ndugu, jamaa na wanachama wa MEWATA waupokee msiba huu KWA UNYENYEKEVU na UTULIVU, tunaomba wamshukuru mwenyezi Mungu kwa muda wote aliowapa kuishi na kushirikiana na marehemu katika harakati mbalimbali za kijamii,tunaomba pia wanachama wa MEWATA waendeleze juhudi za marehemu pale alipoachia na Mungu awape subira katika kipindi hiki kigumu.  Bwana ametoa, bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe, na ampe raha ya milele marehemu, apumzike kwa amani, AMEN    Edda Sanga Mkurugenzi Mtendaji

Viewing all articles
Browse latest Browse all 40

Trending Articles