Quantcast
Channel: TAMWA - TAMWA - PRESS RELEASE
Viewing all articles
Browse latest Browse all 40

TAMWA: SHERIA NA KANUNI ZA USALAMA BARARANI ZIREKEBISHWE ILI ZIWALINDA WANAWAKE NA WATOTO

$
0
0
Chama cha Wanahabari wanawake Tanzania -TAMWA kinaungana na Watanzania katika maadhimisho ya wiki ya usalama barabarani ambayo yataanza tarehe 26/09 na kufikia kilele tarehe 01/10. TAMWA inawaasa wadau wa usalama barabarani kuadhimisha wiki hii kwa kupaza sauti na kutoa wito wa kufanyiwa marekebisho ya sheria na kanuni za usalama barabarani hasa 'Sheria ya Usalama Barabarani ya mwaka 1972. Maeneo ambayo yanapaswa kuzingatiwa katika marekebisho ni mwendo kasi, ulevi wakati wa uendeshaji, uvaaji kofia ngumu, kufunga mikanda na vizuizi kwa watoto. Kutokana na idadi kubwa ya vifo na ajali  barabarani ambavyo hutokea kwa kiwango cha kutisha nchini.  TAMWA inaona kuna umuhimu wa kuchukulia jambo hili kama dharura kwa kuzifanyia marekebisho sheria na kanuni za usalama barabarni ili kuipa nguvu sheria hiyo kuwadhibiti wanaokiuka matumizi sahihi ya barabara. Kwa mujibu wa takwimu za kamanda wa Kikosi cha usalama barabarani nchini, Muhammed Mpinga  zinasema kuanzia Januari hadi Julai,2016,  watu 1580 wamekufa kutokana na ajali barabarani, wengine 4659 walijeruhiwa katika ajali  5152 zilizotokea nchi nzima.  Waliokufa kutokana na ajali za pikipiki ni 430, waliojeruhiwa ni 1,147 katika ajali 1356.  Na takwimu za shirika la Afya Duniani (WHO) Watu milioni 1.25 hufariki kila mwaka Kwa ajali za barabarani.   TAMWA inatambua kwamba wanawake wengi na watoto ndio wenye kubeba mzigo mkubwa unaotokana na ajali barabarani, ingawa takwimu zinaonyesha kuwa  waathirika wa juu wa usalama barabarani ni wanaume. Ila ukweli ni kwamba wanawake na watoto ndio wanaoathirika zaidi kwani watoto hukosa huduma na mahitaji  ya msingi baada ya kupoteza watu wanaowategemea. Edda Sanga, Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA anasema "Umoja wa Mataifa na Shirika la Afya Duniani wanakiri kwamba sheria  madhubuti zinahitajika katika kupunguza idadi ya watu wanaokufa katika barabara zetu. Tanzania lazima tuwe na sheria kali za usalama barabarani kukomesha hali hii ". Kauli mbiu ya wiki ya usalama barabarani mwaka huu ni  "Hatutaki ajali barabarani - Tunataka kuishi salama”. Edda Sanga Mkurugenzi Mtendaji

Viewing all articles
Browse latest Browse all 40

Trending Articles