Quantcast
Channel: TAMWA - TAMWA - PRESS RELEASE
Viewing all articles
Browse latest Browse all 40

UKEKETAJI NA NDOA ZA UTOTONI BADO NI TATIZO NCHINI

$
0
0
Utafiti umebaini kuwa ukeketaji na ndoa za  utotoni bado unaendelea nchini licha ya juhudi zinazofanywa na taasisi mbalimbali za haki za binadamu zikishirikiana na kiserikali .   Novemba mwaka 2015, Chama cha waandishi wa habari wanawake  Tanzania– TAMWA  kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughuliakia idadi ya watu Duniani (UNFPA) kilifanya utafiti wa kihabari wenye lengo la kutathmini hali ya ukatili wa kijinsia kwa kuangalia zaidi  ndoa za utotoni  na ukeketaji kutoka mikoa 13 ya Tanzania Bara na Zanziba. Mikoa hiyo ni Dodoma, Morogoro, Mara, Singida, Shinyanga, Pwani, Dar es Salaam, Arusha, Tabora, Mwanza ,Manyara, Unguja na Pemba.   Takwimu za utafiti zimebaini kuwa kuanzia Januari hadi Oktoba 2015 katika Wilaya ya  Kondoa asilimia 39.9 ya wanawake wajawazito walifanyiwa ukeketaji. Katika Wilaya ya Tarime kesi 118 za ubakaji ziliripotiwa Mahakamani, wakati Pemba wasichana wadogo  240 walipata mimba mwaka 2015. Katika Wilaya ya Mkalama wanawake 2,265 ambao walijifungua katika vituo vya matibabu 115 walifanyiwa ukeketaji. Aidha katika Kata ya Msalala Wilayani Kahama wasichana 605 ambao ni sawa na asilimia 47.47 kati ya 1,150 hawakumaliza shule za sekondari kwa sababu ya Ndoa ya utotoni. Aidha  katika wilaya ya Bagamoyo wasichana 12 wa shule waliripotiwa kupata mimba ndani ya miezi sita kuanzia Januari hadi Juni 2015.
    Utafiti huu umebaini kuwa baadhi ya jamii zimeanza kubadili  mbinu na kubuni mikakati mipya inayowaruhusu  kudumisha mila zao potofu. Moja wapo ya mbinu mbadala  inayotumika ila kufanikisha ukeketeji ni kuwahamisha wasichana kutoka nyumbani kwao na kuwapeleka maeneo ya mbali ili wanajamii  wasitambue kinachoendelea.   Katika maeneo mengine kama Tarime  wao huwapaka wasichana unga usoni ikimaanisha kuwa wao hawakeketwi tena lakini ukweli ni kwamba wamewakeketwa  na kufanya hivyo ni kuficha ukweli.   Kwa upande wa ndoa za utotoni utafiti umebaini kuwa ndoa nyingi za utotoni chanzo kikubwa ni wazazi na ndugu kwa lengo la kupata mahari. Zaidi ni kuwa wazazi wamekuwa wakiwashauri watoto wao kujifelisha mitihani ili iwe sababu ya wao kuolewa. Aidha tafiti imegundua visababishi sugu vya ukeketaji na ndoa za utotoni kuwa ni  pamoja na mila, tamaduni na desturi potofu, umaskini uliokithiri, kukosekana kwa uelewa juu ya haki za binadamu, mfumo dume, ukosefu wa sera imara pamoja  na sheria dhaifu ambazo utekelezaji wake hauridhishi, ukosefu wa mabweni, wanafunzi kutembea umbali mrefu hadi shuleni na mwamko mdogo wa wazazi juu ya umuhimu wa kuwaelimisha watoto wa kike.   TAMWA inaamini kwamba, vyombo vya habari ni daraja la mabadiliko katika jamii kwa kushirikiana na viongozi wa dini, serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali katika kutekeleza  jukumu kubwa la kuhakikisha kuna ulinzi wa  watoto wa kike. TAMWA pia inaamnini vyombo vya habari vinachochea uandishi unaosukuma watu kuyasikiliza yale yanayostawi na maendeleo chanya.   Kupata utafiti kamili tembelea http://www.tamwa.org/.        Edda Sanga Mkurugenzi Mtendaji

Viewing all articles
Browse latest Browse all 40

Trending Articles