Quantcast
Channel: TAMWA - TAMWA - PRESS RELEASE
Viewing all articles
Browse latest Browse all 40

TAMWA YAMLILIA MWANACHAMA WAKE, SARAH DUMBA

$
0
0
Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania –TAMWA kimepokea kwa masikitiko msiba wa mwanachama wake na mwanahabari mahiri, mkongwe Sarah Dumba ambaye amefariki dunia ghafla usiku wa kuamkia leo akiwa wilayani Njombe mkoani Njombe.   TAMWA inaungana na familia ya marehemu Sara Dumba, Serikali, wanahabari na Watanzania wote kwa ujumla katika  kuombeleza kifo hicho kwani ameacha pengo kubwa kwenye taasisi ya wanahabari hasa wanawake na taifa kwa ujumla kutokana na kuwa alifanya kazi zake kwa umakini na weledi wa kuigwa.   Sara Dumba amewahi kuwa mtangazaji wa Radio Tanzania Dar es Salaam- (RTD), Taasisi ya Utangazaji Tanzania (TUT) ambayo kwa sasa inajulikana kama Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), alivuma katika kipindi cha Majira na vipindi vingine vingi. Mwaka 1998 aliteuliwa kuwa mwakilishi wa Mkurugenzi wa Radio Tanzania mkoani Morogoro na baadaye kuhamishiwa Dodoma. Mwaka 2006 Bi Sara aliteuliwa na Rais wa awamu ya nne kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kilindi mkoani Tanga na baadaye alihamishiwa Wilayani Njombe mpaka umauti unamkuta.   Aidha Marehemu Sara Dumba kitaaluma alisomea mafunzo ya Utangazaji  huko Cairo, Misri, pia alipata mafunzo kutoka chuo cha Diplomasia kurasini nchini Tanzania. TAMWA inautambua na  kuuenzi mchango mkubwa wa  marehemu Sarah Dumba hasa  katika  kuhakikisha taasisi ya wanahabari wanawake inafanya tafiti mbalimbali za kihabari kwa kushirikiana na waandishi wa vyombo vyote nchini na kuchapisha ama kutangaza habari zenye kuelimisha na kuhamasisha umma katika kukomesha vitendo vya unyanyasaji na ukiukwaji wa haki za binadamu hasa kwa wanawake na watoto nchini.   Hakika kifo cha Sara Dumba ni pengo kubwa kwa TAMWA, tasnia ya habari, Jamii na taifa kwa ujumla na tunaamini kuwa kazi  nzuri alizozifanya marehemu Sarah na mema yote aliyotenda sehemu mbalimbali vitaendelea kukumbukwa daima. Mungu ailaze kwa amani mahali pema peponi roho ya marehemu Bi Sarah Dumba na kuwatia nguvu na roho ya subira wote walioguswa na msiba huu. AMINA     Edda Sanga Mkurugenzi Mtendaji

Viewing all articles
Browse latest Browse all 40

Trending Articles